Kimataifa

Bobi Wine amtaka Museveni kuwajibika

Bobi Wine amtaka Museveni kuwajibika

Kimataifa
Mbunge maarufu nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, anataka Rais Yoweri Museveni kuwajibika kwa wananchi anao waongoza na kukomesha dhulma na mauaji yanayo "fanywa" na maafisa wa usalama dhidi ya raia. Bobi Wine ametoa wito huo wa moja kwa moja kwa Rais Museveni, wakati serikali ya Marekani ikitaka mashataka ya uhaini dhidi ya Bobi Wine na wenzake 32 kufutiliwa mbali. Tamko la serikali ya Marekani Serikali ya Marekani inaitaka serikali ya Uganda kufutilia mbali mashtaka ya uhaini dhidi ya Mbunge Bobi Wine na wenzake 32, ikisema kwamba mashtaka hayo ni ya kupangwa. Baraza la Wawakilishi Marekani, limemwandikia barua balozi wa Uganda nchini Marekani, Mull Katende likitaka uchunguzi wa kina na usioegemea upande wowote ufanyike, kubaini aliyekos...
Wahamiaji haramu 108 wakamatwa  Kırklareli Kaskazini-Magharibi mwa Uturuki

Wahamiaji haramu 108 wakamatwa Kırklareli Kaskazini-Magharibi mwa Uturuki

Kimataifa
Wahamiaji 108  wamekamatwa na kikosi cha kulinda mipaka Pınahisar, Vize, Kofçaz wakajijaribu kuingia kinyume cha sheria nchini Bulgaria. Wahamiaji hao walikuwa wakijiandaa kuingia   nchini Bulgaria kama hatua yao ya kwanza  kuingia barani Ulaya. Wahamiaji hao waliokamatwa ni raia kutoka nchini Pakistani. Baada ya kukamatwa wahamiaji hao walipelekwa katika  ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kusajiliwa. mkaoni Van, wahamiaji wengine 67 wamekamatwa  baad ya msako mkali wa jeshi la Polisi.     CHANZO: TRT
Tuzo mbadala ya Nobel yatunukiwa Wasaudi Arabia

Tuzo mbadala ya Nobel yatunukiwa Wasaudi Arabia

Kimataifa
Wanaharakati watatu wa haki za binadamu kutoka Saudia walioko jela watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel na taasisi ya Nobel mjini Stockholm. Pia wapinga rushwa kutoka Guatemala watunukiwa tuzo ya heshima. Washindi wa tuzo maalum ya haki za binadamu au tuzo mbadala ya Nobel wametangazwa leo hii mjini Stockholm Sweden. Tuzo hiyo imetunukiwa watetezi watatu wa haki za binadamu wakisaudi waliofungwa jela pamoja na wanaharakati wa kupinga rushwa kutoka Amerika Kusini. Taasisi ya tuzo hiyo mjini Stolkholm imesema dolla 113,400 zinazoambatana na tuzo hiyo mbadala ya Nobel zitagawanywa kwa washindi Abdullah al Hamid,Mohammad al-Qahtani na Waleed Abu al Khair wote wa Saudi Arabia kutokana na juhudi zao za kijasiri zinazosimamia misingi ya haki za binadamu ya kimataifa,ili kuleta mageuzi katik
Homa ya dengu yaikumba Thailand na kusababisha vifo vya watu 71

Homa ya dengu yaikumba Thailand na kusababisha vifo vya watu 71

Afya, Kimataifa
Homa ya dengu imelipuka na kusababisha vifo vya watu 71 nchini Thailand 2018. Ripoti hiyo imetolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo. Kulinga na wizara ya afya nchini humo, zaidi  ya watu 57,000 katika mikoa 27 tofauti wameatirika na ugonjwa huo toka mwezi Januari. Idadi ya vifo kutoka na homa hiyo imeongezeka mara mbili ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2017. Homa hiyo husambazwa na mbu na inaweza kusababisha kifo. Kesi za homa ya dengu huongezeka kati ya Juni-Septemba na Desemba-Machi kulingana na misimu ya mvua. Wanasayansi wameonya kuwa kuongezeka kwa joto na mvua husababisha ongezeko la mbu hali inayosababisha ugonjwa wa Malaria na homa ya dengu kuongezaka.
error: Content is protected !!