International

NATO yaunga mkono mashambulizi ya Marekani Syria

NATO yaunga mkono mashambulizi ya Marekani Syria

International
Shirika la kujihami la Magharibi la NATO lafahamisha kuunga mkono mashambulizi yanayoendeshwa na jeshi la anga la Marekani kwa ushirikiano na Ufaransa na Uingereza nchini Syria. Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema kuwa muungano wa NATO unaunga mashambulizi dhidi ya ghala ambazo zinaamika kuwa na silaha za kemikali nchini Syria. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa NATO, mashambulizi hayo  yatapelekea kwa kiasi kikubwa  kuathiri uwezo wa jeshi la Assad kuweza kushambulia raia kwa kutumia silaha zake za kemikali. Katibu mkuu wa NATO ameendelea kusema kuwa  washirika walikwisha kemea matumizi ya silaha za kemikali hapo awali ni kufahamisha kuwa ni kinyume na makubaliano ya kimataifa.  
Binti mfalme atupwa jela Dubai

Binti mfalme atupwa jela Dubai

International
Mfalme Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum, babake Sheikha Latifa Watetezi wa haki za binaadamu walioko mjini London wametoa wito kwa serikali ya Falme za kiarabu kutoa maelezo ya nini kilichomkuta bintimfalme ambaye amerusha video akieleza namna babake, mfalme wa Dubai , anavyotishia maisha yake . Kikundi hicho kimewekwa kizuizini huko Dubai kimesema kuwa Latifa al-Maktoum alikuwa akijaribu kutoroka himaya ya babake kwa kutumia jahazi lililokuwa na linapeperusha bendera ya Marekani, baada ya kuingia katika bahari ya kimataifa mwezi uliopita wakiwa na walinzi wa bahari ya Hindi. Inaarifiwa kuwa Sheikha Latifa na watu wengine watano walichukuliwa kwa nguvu kutoaka katika jahazi hilo na kuhojiwa kwa muda wa wiki mbili. Na watu wengine waliachiliwa bila mushkeli ingawa binti huyo haju...
Sauti ya Amerika yashinda tuzo 2 maonyesho ya kimataifa

Sauti ya Amerika yashinda tuzo 2 maonyesho ya kimataifa

International
Mzalishaji Mwandamizi wa Habari VOA Beth Mendelson (Kati) na Kutoka kushoto Mhariri Mtendaji wa idhaa ya VOA Hausa, Aliyu Mustapha, Mkurugenzi wa Idara ya Africa, Negussie Mengesha, Mpiga picha Fati Abubakar and Mhariri wa Habari za Uchunguzi VOA,Tom Detzel. Sauti ya Amerika imeshinda tuzo mbili ya dhahabu na shaba za kimataifa wakati wa maonyesho ya kimataifa ya televisheni na filamu mwaka 2018 katika maonyesho ya Jumuiya ya taifa ya watangazaji huko Las Vegas April 10, 2018. “Ninafahari kubwa kwa washindi wetu,” amesema Mkurugenzi wa VOA, Amanda Bennett. “Mafanikio haya yanaonyesha upeo wa vipaji na umahiri ulionyeshwa na waandishi wetu ambao wanafanya kazi kwa bidi kila siku, katika mazingira hatarishi kwa maisha yao, kuuletea ulimwengu wa wafuasi wetu habari mpya, za u
Ajali ya ndege Algeria yauwa 257

Ajali ya ndege Algeria yauwa 257

International
Ndege iliyoanguka nchini Algeria kabla ya kupata ajali. Ndege ya kijeshi ya Algeria iliyokuwa imebeba wanajeshi imeanguka Jumatano asubuhi na kuuwa watu 257. Maafisa wamesema kuwa ndege hiyo imeanguka karibu na kituo cha ndege za kijeshi cha Boufarik muda mfupi baada ya kuruka. Wizara ya ulinzi ya Algeria imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea kwenye eneo la Tindoufkusini mashariki mwa taifa hilo. Mpaka wakati huu sababu za kuanguka ndege hiyo hazijaweza kufahamika.
error: Content is protected !!