Business

Sekta binafsi Zanzibar yajadili mikakati madhubuti ya kufanikisha wiki ya Tanzania nchini Kenya

Sekta binafsi Zanzibar yajadili mikakati madhubuti ya kufanikisha wiki ya Tanzania nchini Kenya

Business
Waziri Wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum akizungumza katika ufunguzi wa mkutano na Wafanyabishara wa Zanzibar uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko tarehe 13 Aprili 2018. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Katibu wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya maonesho ya bidhaa za Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega. Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri Amina aliwasisitiza wafanyabiashara hao kushiriki katika maonesho pamoja na umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa viten...
Bunge la Marekani lailazimisha Facebook kuthibitisha udhibiti wa siri

Bunge la Marekani lailazimisha Facebook kuthibitisha udhibiti wa siri

Business, Science & Technology
Mark Zuckerberg Wabunge wa Marekani wakiwa Washington walimbana kwa maswali magumu Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg wiki hii wakitaka aeleze jinsi kampuni yake ilivyokuwa ikitunza taarifa na siri za watumiaji wa mtandao wake. Pia walipendekeza njia mpya ambazo wanaweza kuzitumia wao au wengine kudhibiti makampuni ya mitando ya jamii. Mark Zuckerberg alikuwa amekabiliwa na maswali magumu ambapo wabunge wa Bunge la Marekani- Congress walitaka majibu ya maswali hayo. Marsha Blackburn Mrepublikan amesema: “Nafikiri kile ambacho tumekifikia hapa, ni nani anaye kumiliki unapokuwa katika mitandao? Nani anamiliki haki zako unapokuwa mitandaoni? Zuckerberg alimjibu mbunge huyo kwamba, “Naamini kuwa kila mtu anamiliki taarifa zake mwenyewe. Na hilo ndio sual
Hahn Air yaibeba ATCL

Hahn Air yaibeba ATCL

Business
NA ABDI SHAMNAH KAMPUNI  ya Ndege Tanzania (ACTL) imetiliana saini mkataba wa makubaliano na Shirika la Ndege la Hahn Air, kutoka jiji la Frankfurt nchini Ujerumani, utakaowezesha  kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa tiketi kupitia mfumo wa kimataifa. Hatua hiyo inafuatia Tanzania kufutwa katika mfumo huo, kutokana na deni kubwa linalodaiwa na Shirika la Ndege Duniani (AITA). Mkataba huo wa miaka mitano umetiwa saini jana katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort, wakati upande wa ATCL uliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Ladislaus Matindi, huku Hahn Air, ikiwakilishwa an Makamu Rais wa Shirika hilo Steve Knackstedt. Akizungumza katika hafla hiyo, Matindi alisema  kutiwa saini kwa mkataba huo kutaiwezesha Tanzania (ATCL), kupata fursa ya kuingia katika mfumo huo Kimataifa, kup
Mafuta yapanda bei Zanzibar

Mafuta yapanda bei Zanzibar

Business
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), imesema kuwa bei za mafuta kwa bidhaa zote kwa mwezi Aprili 2018 zimepanda ikilinganishwa na bei za bidhaa hizo katika mwezi uliopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania. Akizungumza na vyombo vya habari na kutangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika April1 11 ofisini kwake Maisara, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Khudhaimat Bakar Kheir, alisema miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia. Aidha sababu nyengine ni kupanda kwa gharama za ‘Demurrage charges’ na kupanda kwa gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salam kuja Zanzibar. Sababu nyengine alisema ni kupanda kwa gharama za uhifadhi wa mafuta katika bandari ya D
Jinsi wadukuzi walivyoiba bilioni 21 Kenya

Jinsi wadukuzi walivyoiba bilioni 21 Kenya

Business, Science & Technology
Noti za pesa za Kenya zilizochapishwa kwa mfumo wa 3D Dola za Marekani milioni 210 ziliibwa na wadukuzi kutoka kwenye Benki na Taasisi za serikali nchini Kenya mwaka 2017. Hii ni kwa mujibu w ripoti ya shirika la usalama mitandaoni, SERIANU, ambayo inasema mataifa ya bara la Afrika yalipoteza jumla ya dola milioni 350. Ikizingatiwa kwamba, kati ya mwezi Januari na mwezi Februari mwaka jana, Kenya ilipoteza dola milioni 50 kwa wadukuzi, ni wazi kwamba usalama wa fedha za wateja wa benki haujazingatiwa na benki nyingi. "Udukuzi ni uhalifu unaobadilika kila kunapokucha" anasema Delano Kiilu, mtaalamu wa masuala ya usalama mitandaoni. Kutoka kushoto: Mkurugenzi mkuu wa Serianu Limited, William Makatiani, Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Balozi Raychel Omamo na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Maml...
error: Content is protected !!