Bulletin & Updates

Bulletin & Updates

Serikali kusimamia utunzaji mazingira

Serikali kusimamia utunzaji mazingira

Bulletin & Updates
NA MWASHAMBA JUMA KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Khadija Bakari Juma, amesema wizara hiyo ni mdau mkuu wa kutunza mazingira kupitia taasisi zake za utalii na mambo ya kale. Aliyasema hayo ofisini kwake Kikwajuni wakati akizungumza na kamati ya taifa ya ZNSC, inayosimamia mradi wa ikolojia kwa skuli za Unguja na Pemba (Eco Schools) pamoja na ujumbe kutoka ZAYEDESA uliofika ofisini kwake kwa ajii ya kuutambulisha mradi mpya wa misingi kwa ajili ya elimu na mazingira (FEE), ambao unatarajiwa kufanyakazi kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia taasisi zake za utalii, mazingira na elimu na taasisi binafsi zinazosimamia utunzaji wa mazingira nchini. Alisema ana uzoefu na kuufahamu mradi huo tokea alipokua Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na sa...
Obama, viongozi chipukizi wamuenzi Nelson Mandela Afrika Kusini

Obama, viongozi chipukizi wamuenzi Nelson Mandela Afrika Kusini

Bulletin & Updates
Katika kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi, Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, alikutana na viongozi chipukizi mjini Johannesburg kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kuadhimisha siku hiyo. Katika kuadhimisha siku hiyo Jumatano wananchi wa Afrika Kusini hujishughulisha na kazi za kujitolea. Siku moja kabla ya maadhimisho hayo, Obama ambaye pia ni Rais wa kwanza mweusi alitoa hotuba ambayo inawezekana ilikuwa ni tamko lenye uzito mkubwa kuliko yote aliyotoa tangu amalize kipindi chake cha urais. Kaitka hotuba yake siku hiyo ya kumbukumbu, inayofanyika kila mwaka kumuenzi Nelson Mandela, Obama alitoa sifa nzuri ya maendeleo na usawa yalioletwa na viongozi kama vile Marehemu Mandela, na kisha kulinganisha na kile alichokiita sia...
Mwanamke afariki akiongezwa ukubwa wa makalio nchini Brazil

Mwanamke afariki akiongezwa ukubwa wa makalio nchini Brazil

Biashara & Uchumi, Bulletin & Updates, Kimataifa, Tehama
Dokta Denis Furtado ana takriban wafuasi 650,000 kwenye ukurasa wa Instagram Daktari wa ubadilishaji viungo anayefahamika kwa jina la Dokta Bumbum ametoroka baada ya kusababisha kifo cha mwanamke mmoja aliyemchoma sindano kwa ajili ya kukuza makalio. Wapelelezi wanasema dokta Denis Furtado alifanya kitendo hicho kwa Lilian Calixto katika makazi ya daktari huyi Rio de Janeiro, lakini aliungua wakati wa mchakato huo. Dokta Furtado alimpeleka hospitali ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na akapoteza maisha, saa kadhaa baadae, Polisi alieleza. Kisha alitoweka na Jaji ametoa waranti ya kuwezesha kukamatwa. Dokta Furtado alionekana kwenye Televisheni ya nchini Brazil na ana wafuasi takriban 650,000 kwenye mtandao wake wa Instagram. Bi Calixto, mwenye miaka 46, mwenye ndoa na wa...
Maradhi ya Ebola kutokomezwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ifikapo Julai 25

Maradhi ya Ebola kutokomezwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ifikapo Julai 25

Bulletin & Updates, Tehama
Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kutokomezwa maradhi ya Ebola nchini humo ifikapo tarehe 25 ya mwezi huuu wa Julai. Taarifa ya wizara hiyo imebainisha kwamba, nchi hiyo inasubiri kwa hamu tarehe 25 ili kutangaza kutokomezwa kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo iwapo kutakuwa hakujaripotiwa kesi mpya ya maambuzi ya ugonjwa huo. Hii inatokana na ukweli kwamba, tangu tarehe 12  mwezi uliopita hadi jana hakuna kisa chochote kipya cha Ebola kilichoripotiwa na hivyo ikifika tarehe 24 mwezi huu bila kuripotiwa kesi mpya ya ugonjwa huo basi vita dhidi ya mlipuko wa Ebola  ulioanza tarehe 8 mwezi Mei mwaka huu vitakuwa vimefanikiwa, imeeleza sehemu nyingine ya taarifa hiyo. Akizungumza na waandishi  habari mjini Geneva, Usiwisi, Fad
Salva Kiir na Riek Machar kutia saini mkataba wa amani Alkhamisi ya kesho

Salva Kiir na Riek Machar kutia saini mkataba wa amani Alkhamisi ya kesho

Bulletin & Updates
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imetangaza kuwa, pande hasimu nchini Sudan Kusini zimefikia makubaliano ya kugawana madaraka ambayo yatatiwa saini Alkhamisi ya kesho. Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na hasimu wake, Riek Machar kesho wanatarajiwa kutiana saini makubaliano ya awali ya kugawana madaraka kabla ya mkataba wa mwisho tarehe 26 mwezi huu. Pande hasimu Sudan Kusini zimeafiki kugawana madaraka kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo ambapo kwa mujibu wake kiongozi wa waasi nchini humo, Riek Machar atarejeshwa katika wadhifa wake wa awali wa Makamu wa Rais. Hivi karibuni Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan ilitangaza kuwa, imeafikiwa kwamba kutakuwepo Makamu wanne wa Rais; yaani Makamu wawili wa Rais waliopo hivi sasa pamoja
Ripoti: Askari vamizi wa Imarati wanawateka na kuwabaka wanawake wa Yemen

Ripoti: Askari vamizi wa Imarati wanawateka na kuwabaka wanawake wa Yemen

Bulletin & Updates
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kwamba, vitendo vya kutekwa nyara wasichana wa Yemen na kubakwa katika maeneo yanayodhibitiwa na askari vibaraka na vamizi wanaoungwa mkono na kufadhiliwa na serikali ya Imarati, vimeongezeka zaidi. Baadhi ya ripoti zinaeleza kwamba, wiki iliyopita wasichana wawili walio na umri wa chini ya miaka 20, walitekwa nyara na askari wanaoungwa mkono na serikali ya Abu Dhabi na kuwabaka. Wazazi wa wasichana hao pia walitishiwa usalama wao kwamba, iwapo watafichua watu waliowateka nyara watoto wao, watauawa. Kwa mujibu wa taarifa zilizoufikia mtandao wa habari wa Murasil Net, askari wa Imarati wanasimamia kundi la maafisa kadhaa wa usalama vibaraka ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kuwateka nyara mabinti wa Yemen na kisha kuwakabidhi kwa askari hao vam
Rais Magufuli ateuliwa mshindi wa Tuzo ya Ukombozi Afrika

Rais Magufuli ateuliwa mshindi wa Tuzo ya Ukombozi Afrika

Bulletin & Updates
Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi. Mwebesa Rwebugia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Ukombozi Afrika, ametangaza kuwa, Rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasa katika ukuaji wa miundo mbinu. Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika. Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa, katika kuegemea kwenye muktadha wa uchumi, kamati iliangalia umaskini ambao unatajwa kuwa adui mkubwa anayefahamika, lakini pia maradhi na ujinga. Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika, ukombozi katika kipengelee cha elimu huangazia elimu na ujinga ka
Janga la mafuriko laua makumi ya watu Nigeria

Janga la mafuriko laua makumi ya watu Nigeria

Bulletin & Updates
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Nigeria yameua watu zaidi ya 49, na wengine 20 bado hawajulikano waliko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Niger. Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa, makumi ya nyumba zimebomolewa na kusombwa na maji kufuatia janga hilo la mafuriko huku mifugo wasiopungua 260 wakiwemo ng'ombe. mbuzi na kondoo wakiangamizwa. Rais Muhamadu Buhari wa nchi hiyo amesema kuwa, serikali itafanya kila iwezako kuhakikisha kuwa, waathirika wa mafuriko hao wanapatiwa misaada ya haraka. Aminu Waziri, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Dharura katika Jimbo la Katsina amewaambia waandishi wa habari kwamba, hadi sasa miili ya wahanga 49 waliopoteza maisha katika janga hilo la mafuriko imepatikana. Hata hivyo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Dharura amesema kuwa, kuna
Watu wanne wakamatwa wakihusishwa na mauaji ya mwanafunzi

Watu wanne wakamatwa wakihusishwa na mauaji ya mwanafunzi

Bulletin & Updates
KAMPALA, UGANDA POLISI jijini Kampala wanawashikilia watu wanne kwa mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Mashariki raia wa Sudan Kusini. Msemaji wa Polisi Kampala, Luke Owoyewogyire alisema watu hao walikamatwa Alkhamis baada ya mauaji ya kikatili ya kijana Lam Duot Deng Duot Juni  23, 2018. “Wanahusishwa na mauaji ya raia wa Sudan Lam Duot Deng Duot, aliyeuawa na kundi la wazoaji taka,” alisema. Kwa mujibu wa Polisi , Duot alishutumiwa kutaka kumuibia mama mmoja na pia alishutumiwa kuhusika katika vitendo vya jinai katika eneo hilo. Polisi  walisema binamu wa Duot alitoa taarifa ya kutoweka kwalke na kushauriwa kumtafuta katika chumba cha kuhifadhia maiti Mulago ambapo mwilMashuhuda walieleza jinsi ya washukiwa hao walio na umri baina ya miaka 20 na 3
Besigye: Kushiriki uchaguzi Uganda ni kupoteza wakati

Besigye: Kushiriki uchaguzi Uganda ni kupoteza wakati

Bulletin & Updates
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye Akiwa kwenye ziara ya siku mbili nchini Kenya, kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, alisisitiza kauli yake ya awali kwamba utawala wa rais wa taifa hilo, Yoweri Kaguta Museveni, unaendelea kuwakandamiza wananchi wake. Besigye, ambaye alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika siku ya Jumanne katika mahojiano ya kipekee jijini Nairobi, alisema kuwa haupo umuhimu wowote kwa raia wa Uganda kushiriki uchaguzi "ambao unafanyiwa ukarabati na wandani wa Museveni." Na kutokana na hayo, mwanasiasa huyo alisema ni sharti sasa raia wa Uganda wahimize mabadiliko muhimu katika taasisi muhimu nchini humo. La sivyo wataendelea kutekwa nyara na kiongozi huyo ambaye amekaa madarakani zaidi ya miaka thela...
error: Content is protected !!