Biashara & Uchumi

Wito wa Somalia kwa wawekezaji wa kigeni kuwekeza katika forodha  ya mjini Mogadishu

Wito wa Somalia kwa wawekezaji wa kigeni kuwekeza katika forodha ya mjini Mogadishu

Biashara & Uchumi, Kimataifa
Somalia inayo matumaini makubwa kufungua forodha  yake ya mjini Mogadishu  kwa kutoa wito kwa wawekezaji wa kigeni. Inafahamika kuwa forodha ya mjini Mogadishu ilikuwa na umuhimu mkubwa katika shuhuli za uchukuzi kati ya eneo hilo la pembe ya Afrika kuelekea katika mataifa tofauti barani Ulaya tangu miaka ya 1960. Hali ilibadilika tangu mwaka 1991 wakati ambapo kulizuka mapigano. Uongozi wa forodha nchini Somalia  baada ya kuona kuwa  usalama unazidi kuimarika umetolea wito wawekezaji kuwekeza katika  sekta hiyo.
Serikali ya Benin yaondoa kodi ya mitandao ya kijamii

Serikali ya Benin yaondoa kodi ya mitandao ya kijamii

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa
Serikali  ya Benin yaondoa kodi  iliokuwa imewekwa  kwa ajili ya mitandao ya kijamii. Serikali ya Benin yachukuwa aumuzi wa  kuondoa kodi iliokuwa imewekwa kwa ajili ya mitandao ya kijamii. Sheria hiyo kuhusu mitandao ya kijamii iliwekwa  Julai. Raia nchini humo waliandamana kupinga sheria hiyo na kuishinikiza  serikali kuondoa sheria hiyo. Rais wa Benin Patrice Talon  na wizara inayohusika na mitandao wamefahamisha katika kurasa zao  kuwa sheria hiyo ya kutoza kodi  mitandao ya kijamii imeondolewa.
Mapigano yaanza tena karibu na matangi ya mafuta huko Tripoli, Libya

Mapigano yaanza tena karibu na matangi ya mafuta huko Tripoli, Libya

Biashara & Uchumi, Kimataifa
Duru za kiusalama za Libya zimetangaza habari ya kuanza tena mapigano kandokando ya matangi ya mafuta huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo. Mapigano hayo yameripotiwa kujiri kati ya makundi yenye silaha nzito karibu na makao makuu ya matangi ya kuhifadhia mafuta ya Shirika la al Birikha katika barabara iendayo uwanja wa ndege wa Tripoli. Mapigano hayo yamejiri huku kukiripotiwa kuvurumishwa makombora kadhaa pia kuelekea maeneo kadhaa huko Wadi al Riba kusini mwa Tripoli. Mustafa Sanallah Mkuu wa Shirika la Taifa la Mafuta la Libya siku tatu zilizopita alitahadharisha kuhusu kujitokeza tatizo la mafuta kutokana na kuharibiwa sana matangi ya kuhifadhia mafuta na kusema: Hivi sasa yamesalia matangi matatu tu ya mafuta huko Tripoli na kwamba shirika la mafuta pia linakabiliwa na matati
Uturuki yaitaka Venezuela kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani

Uturuki yaitaka Venezuela kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Uturuki imeialika Venezuela kutumia sarafu za nchi zao badala ya dola katika miamala ya kibiashara ya pande mbili; ikiwa ni katika kampeni ya kuimarisha uchumi wa nchi hizo kukabiliana na mashinikizo ya serikali ya rais wa Marekani, Donald Trump.  Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Venezuela Jorge Arreaza, Mevlut Cavusoglu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kama ninavyomnukuu: "Tuna hamu kubwa ya kutumia sarafu za nchi zetu katika biashara ya pande mbili si tu kati ya Uturuki na Venezuela bali pia kati ya Uturuki na nchi nyingine," mwisho wa kunukuu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameongeza kuwa mara nyingi tumekuwa tukijaribu kutumia pesa za nchi zetu katika miamala ya kibiashara kwa kuzingatia kuwa serikali ya Marekani imekuwa ikitumia sarafu ya d
error: Content is protected !!