Barua ya Syria kwa UN kufuatia jinai za muungano wa kijeshi wa Marekani

Barua ya Syria kwa UN kufuatia jinai za muungano wa kijeshi wa Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo ikitaka kuchunguzwa jinai zilizofanywa na muungano vamizi wa kijeshi wa Marekani katika viunga vya mji wa al Bukamal nchini humo.

Ndege za kivita za muungano vamizi unaoongozwa na Marekani jana asubuhi ziliyashambulia maeneo ya raia huko al Baguz Faqani na al Sawsah katika viunga vya al Bukamal mashariki mwa mkoa wa Deir Zor Syria ambapo hadi kufikia sasa raia 53 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Shambulio la muungano vamizi unaoongozwa na Marekani mkoani Deir Zor nchini Syria 

Katika barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeeleza namna muungano unaoongozwa na Marekani usivyoweza kuhahalisha hujuma hiyo ya kinyama na kubainisha kuwa: Mashambulizi hayo yalilenga wanaviji wa al Baguz Faqani na al Sawsah ambao wamekuwa wakipinga kuingia katika vijiji vyao wanamgambo wa kundi linalojiita Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria.

Wanamgambo ambao wanaungwa mkono na muungano unaoongozwa na Marekani wanadhibiti maeneo ya mpaka wa Syria na Iraq katika mkoa wa Hasakah na vilevile eneo la Tanf mashariki mwa mkoa wa Homs huko magharibi mwa Syria.

error: Content is protected !!