Author: PembaLive

Pesa zilizobaki katika  bajeti ya mwaka 2017 nchini Singapore wapewa raia

Pesa zilizobaki katika bajeti ya mwaka 2017 nchini Singapore wapewa raia

Business
Serikali ya Singapore imefahamisha kutoa pesa zilizobaki katika bajeti ya mwaka 2017 kwa raia wake wote  wenye umri wa zaidi ya miaka 21. Raia wote wenye umri wa zaidi ya miak 21  wataongezewa kiwango cha dola 100 hadi 300 katika miishahara yao. Bajeti iliopangwa na kutolewa kwa mwaka 2017 ilitumiwa na kiwango kikubwa cha pesa hakikutumika. Waziri wa fedha wa Singapore Heng Swee Keat amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa  baada ya kuona kuwa bajeti ilikuwa kubwa. Waziri wa fedha amesema kwa serikali ya Singapore inatumikia raia wake na kuwa na lengo la maendelea kwa kila raia wake. Ikumbukwe kuwa Singapore ilitoa kiwango cha dola 100 hadi 800 kwa raia wake mwaka 2011.   CHANZO: TRT
Kamisheni ya wakfu imesema haina uwezo wa kumlazimisha mtu kutoa Zaka

Kamisheni ya wakfu imesema haina uwezo wa kumlazimisha mtu kutoa Zaka

News Bulletin
Kamisheni ya wakfu na mali ya amana imesema haina uwezo wa kumlazimisha mtu kutoa Zaka badala yake watu wenye uwezo wawakumbuke na kuwasaidia watu wasiojiweza kwa kutoa Zaka ili kuwapunguzia ugumu wa maisha. Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar , Naibu Waziri wizara ya katiba sheria utumishi wa Umma na Utawala bora Khamis Mwalimu amesema jukumu la kamisheni hiyo ni kuratibu na kukusanya Zaka zinazotolewa na kuzitowa kwa wananchi waliokusudiwa. Amesema mtu mwenye uwezo wa kutoa Zaka ni vyema kutoa kwa kuzingatia sheria na taratibu za dini au kuwasilisha Zaka yake katika kamisheni hiyo ili iweze kugaiwa kwa wananchi. Aidha Naibu Waziri ametoa wito kwa watu wenye uwezo kuendelea kuwa na imani ya kuwasilisha Zaka zao katika ka...
Kiringo akamatwa kwa tuhuma za kulawiti

Kiringo akamatwa kwa tuhuma za kulawiti

News Bulletin
POLISI Mkoa wa Mjini Magharibi, wamemkamata Hassan Aboud Talib (Kiringo) mwenye umri wa miaka 45, kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 13 jina linahifadhiwa. Kamanda wa polisi mkoa huo, Hassan Nassir Ali, alitoa taarifa hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Madema. Alisema Kiringo ambae ni mfanyakazi wa taasisi moja mapato nchini, alikamatwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akiwa katika harakati za kusafiri kuelekea Mwanza. Alisema mtuhumiwa huyo alitumia hadaa kwa mtoto huyo kwa kumpa dawa za kulevya na kufanikiwa kumfanyia kitendo hicho akiwa hajitambui. Kamanda Nassir alisema baada ya kupata taarifa, walimchukua mtoto aliefanyiwa kitendo hicho na kumpeleka hospitali ya Mnazimmoja kwa uchunguzi ambao ulibaini kufanyiwa kiten...
Achezea kipigo akidaiwa kuwa ni mwizi

Achezea kipigo akidaiwa kuwa ni mwizi

Local
NASSOR Abdalla Nassor (22) mkaazi wa Maziwani, achezea kipigo kutoka kwa wananchi wasiojulikana huko Mzambarauni Patini Wilaya ya Wete akidawa kuwa mwizi. Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema lilitokea Febuari 13 mwaka huu usiku, mara baada ya wananchi wa kijijini hapo kumtuhumu kuwaibia. Alieleza baada ya kupata taarifa hiyo, Jeshi la Polisi Mkoa huo walikwenda kumchukuwa na kumpeleka hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. “Waliompiga kijana huyu mpaka sasa hivi bado hawajulikani walipo, kwa sababu mwenyewe hajataja hata mmoja”, alisema Kamanda huyo. Alieleza   upelelezi bado unaendelea na iwapo watagundulika waliohusika na tukio hilo la shambulio la kuumiza mwili, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. “K
Watu zaidi ya milioni 5 wajiandikisha kupiga kura ya maoni nchini Burundi

Watu zaidi ya milioni 5 wajiandikisha kupiga kura ya maoni nchini Burundi

International
Idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura ya maoni kuhusu marekebesho ya katiba na uchaguzi mkuu wa mawaka 2020 ni watu  5 008 742. Taarifa hiyo ilitolewa hapo Jumatatu na tume ya kitaifa inayosimamia uchaguzi . Kura ya maoni kuhusu marekebesho ya katiba nchini Burundi  inatarajiwa kufanyika  mwezi Mei mwaka 2018. Akizungumza na waandishi wa habari msimamizi wa tume ya kitaifa ya kusimamia uchuguzi Pierre Claver Ndayicariye  amesema kuwa  balozi za Burundi ugenini watu 7 284 wamejiandisha lushiriki katika uchaguzi. Raia wa Burundi walioko Somalia na Jamhuri ya Afrika ya Kati  wapatao  782 na 4 805  ndio ambao wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi. Ifahamike kuwa wanajeshi wa Burundi wanashiriki katika vikosi vya  kimataifa vya kulinda amani nchini Somalia na Jamhu
error: Content is protected !!