Thursday, October 21
Shadow

Author: Editor in Chief

Happy Eid al-Adha – 2021

Happy Eid al-Adha – 2021

Peace and blessings of Almighty Allah be with you all, For and on behalf of Moyo Media Co. Ltd and our subsidiary companies, We want to wish our Muslim clients and all the Muslims of the world on the blessed occasion of Eid al-Adha. May your life be filled with joy, happiness and wisdom. May your family always be healthy and successful and you be surrounded by care and love.
Dk.Hussein Ali Mwinyi ameunga mkono mashirikiano kati ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Dk.Hussein Ali Mwinyi ameunga mkono mashirikiano kati ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

RAIS wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa baraka zake na kuunga mkono mashirikiano yanayoimarishwa kati ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika suala zima la kuimarisha uwekezaji nchini.Rais Dk. Mwinyi ametoa baraka hizo katika mazungumzo aliyoyafanya kati yake na uongozi wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji Shariff Ali Shariff pamoja na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji Dk. Maduhu Isaac Kazi, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar. Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa jambo wanalolifanya na kuendeleza utaratibu wa kukuza mashirikiano ni jambo la busara na lina tija kubwa kati...
Shaibu Foundation yazindua mradi wa elimu mtandao kwa skuli za msingi na sekondari kisiwani Pemba

Shaibu Foundation yazindua mradi wa elimu mtandao kwa skuli za msingi na sekondari kisiwani Pemba

Shaibu Foundation ni taasisi isiyo ya kutengeneza faida iliyosajiliwa Zanzibar, inayojikita katika maeneo mbali mbali ikiwemo elimu. Siku ya Jumamosi ya tarehe 26/06/2021 Shaibu Foundation ilizindua mradi wa elimu mtandao awamu ya pili kwa skuli za msingi na sekondari kisiwani Pemba. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa American Space Pemba. Mafunzo hayo yatafanyika kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu kwa kila skuli itakayonufaika. Ambapo skuli zitatakazonufaika na mradi huo ni Ng’ambwa Sekondari, Mchanga Mdogo Msingi, Mjananza Msingi, Makoongwe Msingi na Sekondari, Msuka Msingi na Sekondari, Vikunguni Msingi na Sekondari, Chasasa Sekondari, Utaani Sekondari na Chuo cha Kiislamu Pemba. Mradi huu ulianza rasmi mnamo mwaka 2018, ambapo kwa awamu ya kwanza walimu wa Skuli...