Al Houthi: Uislamu wa Kimarekani ni wa kinafiki

Al Houthi: Uislamu wa Kimarekani ni wa kinafiki

Katibu Mkuu wa harakati ya Ansurulla nchini Yemen amesema kuwa Uislamu wa Kimarekani, Kisaudia na Kiimarati ni Uislamu wa kinafiki unaopingana na asili ya Uislamu.

Abdul Malik Badruddin al Houthi alisema jana Ijumaa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya Maandamano ya Kupinga Ubeberu kwamba Muislamu wa kweli hawezi kuwa kibaraka wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba misingi na nguzo za dini ya Uislamu hazikubaliani hata kidogo na yale yanayofanywa na Marekani na Israel.

Katibu Mkuu wa Ansarullah amongeza kuwa, harakati za Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati zinafanyika kwa shabaha ya kuudhibiti Umma wa Kiislamu na kwamba tawala hizo mbili zinafanya njama za kutoa pigo kubwa kwa Waislamu.

Abdul Malik Badruddin al Houthi

Ameashiria mpango wa Marekani ulipewa jina la “Muamala wa Karne” unaokusudia kuangamzia kabisa kadhia ya Palestina na kusema: Saudi Arabia ni mshirika mkuu¬†katika njama hiyo hatari na inahudumia malengo ya Wamarekani na Wazayuni.

Abdul Malik al Houthi amesisitiza kuwa, njia pekee ya kujiondoa katika hali hiyo ni nchi za Kiislamu kurejea katika mafundisho ya Qur’ani na kuyatekeleza kivitendo na kwamba suala hilo linawalazimu wafuasi wa dini hiyo kusimama kidete dhidi ya siasa za kibeberu za Marekani.

error: Content is protected !!