TCRA yatoa ufafanuzi kujisajili kwa watumiaji wa mitandao

TCRA yatoa ufafanuzi kujisajili kwa watumiaji wa mitandao

Business
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, imesema, mtumiaji mmoja mmoja wa mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter hatakiwi kujisajili. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, imesema taarifa zinazosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii kwamba watumiaji hao wanapaswa kujisajili ni za uongo. Taarifa hiyo imesema, kanuni zinawataka watumiaji wa mitandao kuwajibika kwa maudhui watakayopakia kwenye mitandao hiyo. Hata hivyo taarifa hiyo imefafanua kwamba, wamiliki wote walio na leseni za utangazaji wanaotumia mitambo iliyosimikwa ardhini endapo watapenda kutumia mitandao hiyo ya kijamii yaani Twitter, Instagram na Facebook kurusha maudhui yao kwa lengo la kujisajili lazima wajisajili kwanza TCRA. Kilaba ameonya kuwa, ma...
Wananchi na Watoto Kijijini Kengeja Kisiwani Pemba Wakiadhimisha Sikukuu ya Eid El Fitry Katika Viwanja vya Skuli Kengeja.

Wananchi na Watoto Kijijini Kengeja Kisiwani Pemba Wakiadhimisha Sikukuu ya Eid El Fitry Katika Viwanja vya Skuli Kengeja.

News Bulletin
"Tulioyarisi na kuyaacha bado yanaendelea kurisiwa,ndugu zangu nikiwa hapa jijiji kwetu Kengeja Kusini Pemba leo nimeshuhudia makundi ya watoto kutoka viunga tofauti vya hapa kijijini kwetu wakiendelea kifurahia sikukuu ya Eid. Eneo hili tulitumia kaka zao siku kama hizi miaka ya nyuma ambapo sisi pia tulirisishwa na kaka na dada zetu leo wadogo zetu nao wanafurahia. Kwa hakika inapendeza na inatia moyo kwa maana tulioyaacha yanaendelezwa."       CHANZO: ZANZINEWS
Watu 16  wafariki kufuatia mvua  kali na mafuriko Kaskazini mwa Nigeria

Watu 16 wafariki kufuatia mvua kali na mafuriko Kaskazini mwa Nigeria

News Bulletin
Watu 16 wamefariki na wengine kadhaa wajeruhiwa   Kaskazini mwa Nigeria kutokana na mvua kali zilizosababisha mafuriko. Kutokana na mvua kali zilionyesha  katika eneo Bauchi, watu 16 wamefariki na wengine  kadhaa kujeruhiwa. Mvua kali zimenyesha usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili zimepelekea baadhi ya vituo vya biashara kufungwa na bidhaa tofauti kuharibika kwa maji. Majumba kadhaa yamebomoka, miti kung'oka  huku hofu  ya mvua kuendelea ikitanda.
Majambazi wanaopora pesa ambao wameishangaza Afrika Kusini

Majambazi wanaopora pesa ambao wameishangaza Afrika Kusini

Business
Milipuko imetumiwa kwenye visa kadhaa vya wizi Takriban kila siku nchini Afrika Kusini, kampuni za kusafirisha hela hulengwa na majambazi wanaowavamia na kuwapora. Hata baadhi ya matukio huhusisha utumiaji wa vilipuzi. Mamilioni ya fedha hutoweka kila siku chini ya mikononi mwa majambazi sugu baadhi yao wakiwa gerezani. Aidha, Maafisa wa polisi wametajwa kuhusika katika baadhi ya wizi. Kipikinaendela? Kumekuwa na visa 378 vya uporaji wa pesa ikimaanisha ongezeko la asilimia 104% kati ya mwaka 2016 na 2017. Huenda hali ikawa mbaya zaidi mwaka huu kwani, kati ya mwezi Mei mwaka uliopita hadi Januari mwaka huu pekee, visa 153 vya uporaji vimeripotiwa ikiwa ni zaidi ya tukio moja kila siku. Usafirishajii wa pesa kutumia magari yasiyopenya risasi haujaboresha hali kwani wezi hao ...
Bomu lawauwa maafisa usalama 8 Kenya

Bomu lawauwa maafisa usalama 8 Kenya

News Bulletin
Kikundi cha kigaidi cha al Shabaab, Somalia Maafisa usalama wasiopungua wanane Jumapili waliuwawa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu katika eneo la Bojigaras, Kaunti ya Wajir. Kwa mujibu wa gazeti la the Standard Digital wahanga hao ni pamoja na Maafisa Utawala wa Polisi watano na polisi watatu wakujitolea. Vyombo vya usalama vimesema kuwa gari walilokuwa wanatumia marehemu hao lilikanyaga bomu la kutengenezwa kienyeji na gari hilo kurushwa angani. Walioshuhudia tukio hilo wamesema gari hilo liliharibiwa vibaya sana na watu wote waliokuwa ndani yake waliuwawa. Mratibu wa eneo la Kaskazini Mashariki Muhammad Saleh amesema wale waliohusika na shambulizi hilo walikimbia mara baada ya tukio hilo. Amesema uchunguzi wa awali unaashiria kuwa waliohus...
error: Content is protected !!