Habari Maelezo waifyagilia Mtandao wa PembaToday

Imeandikwa na Mohd khalfan , Pemba

Mkuu wa Idara habari maelezo Pemba, Marzouk Khamis Sharif amewataka vijana kuutumia mtandao wa mawasiliano wa Pemba Today kufuata taratibu na misingi bora ili kuepuka kusambaza habari zenye kuchafua sifa ya Taifa.

Amesema mitandao ya habari ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa, hata hivyo ni wajibu wa jamii kuitumia teknologia hiyo kwa manufaa badala ya hasara.

Mazrouk ameyasema hayo huko ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kuhusu kuanzishwa mtandao wa vijana wa Pemba unaoitwa Pemba Today.

Amesema kwamba iwapo vijana hawatakuwa na tahadhari ya matumizi ya mitandao kutasababisha kuporomoka maadili sambamba na kuchafua mila, silka na tamaduni za Taifa.

Vijana kisiwani Pemba, wameanzisha mtandao wa mawasiliano unaojulikana Pemba Today wenye lengo la kutoa habari za maendeleo ya kijamii pamoja na kuibua fusa na kupambana na changamoto mbali mbali za kiuchumi.

Vijana hao pia wameiomba Serekali kupitia Idara ya habari Maelezo Pemba kutoa msaada kwa vijana hao ili waweze kutekeleza majukumu ya mtandao wao walio anzisha.

 

 

CHANZO: PEMBA TODAY

error: Content is protected !!