
ZATU wampongeza Rais Shein kwa agizo lake
Chama cha Walimu Zanzibar zatu kimesema utekelezwaji wa agizo alilolitoa Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein juu ya kulipwa walimu wa Zanzibar malimbikizo yao ya uzowefu wa miaka 30 ya kufanyakazi imewapa hamasa na ari walimu kuzidisha kasi ya kufundisha wanafunzi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Katibu Mkuu wa chama hizo Mussa Omar Tafurwa amesema zoezi la ulipwaji wa madeni ya walimu yameshaanza kulipwa kwa walimu pemba na kuwaomba watendaji kuzidisha kasi ya ulipaji wa madeni hayo kwa walimu wa unguja ili na wao waweze kufaidika na fedha hizo.
Tafurwa amesema ulipaji huo wa madeni umeleta faraja kwa walimu kwani kazi wanayoifanya ya kuwafundisha watoto ni kubwa na inataka umakini mkubwa hivyo serikali iyone haja ya kuona umuhimu wa kuwalipa madeni yao wanayodai.